Swahili media DJ PRO awashia moto Mkali wa Show
Mwanamuziki wa kizazi kipya kutoka nchini Burundi anayetambulika kama DJ PRO amewasha moto kwa Msanii mwenzake anayetambulika kama MKALI WA SHOW kupitia wimbo wake mpya uliopewa jina la BLAA BLAA aliomshirikisha EMERY SUN.
Nikukumbushe kuwa tofauti za hawa wasanii wawili zimeanzia kwenye mitandao ya kijamii ila kwa sasa tayari zimefika ndani ya jamii halisia ya BUJA FLEVA na kwa wapenzi wote wa muki wa BUJA FLEVA.

Yanayojiri ni kwamba DJ PRO baada ya kuamshwa na MKALI WA SHOW kwenye tofauti zao sasa ameamua kuingia studio na kuachia wimbo wake mpya ambao unaonyesha fika fika kama ameamua kuwasha moto.

kwenye KIPANDE CHA VERSE YA TATU kuna mistari inasema hivi:
« MKALI WA NINI?
ETI WA SHOW
KWA KITU GANI?
USHAFANYA NINI
TIC TAC KWANZA HUNA FLOW… »
Hicho ndicho ambacho kinamhusu MKALI WA SHOW kwenye wimbo wake DJ PRO.

Kwa kauri yake DJ PRO akifanya mahojiano na mwandishi wa SWAHILI MEDIA amesema kwamba yeye hana noma yoyote ila yuko tayari kuongeza petroli kwenye moto ikiwa MKALI WA SHOW atajibu mapigo hayo.
Usisahau kushare na wengine kama kawaida yetu.

Pakuwa mzigo mzima hapa

Favicon Swahili media DJ PRO awashia moto Mkali wa Show