Swahilimedia Maisha halisi ya SPOKS Man Bio
NDAKUMBUYE IWACU THE ALBUM COVER

Fahamu maisha halisi ya Mwanamuziki kutoka Nchini Burundi SPOKSMAN.

Spoks alizaliwa tarehe 15, April mwaka 1992 katika Hospitali ya Prince Regent Charles iliyopo BURUNDI jijini Bujumbura na kupewa jina la Dushimirimana Eric . Akiwa na umri mdogo wazazi wake walifariki akalelewa Bwiza kwa bibi yake mzaa mama.

Elimu yake ya Msingi yaani (Primary School) alianza mwaka 1999 katika shule ya msingi Saint Michel iliyopo jijini Bujumbura. Ilipofika mwaka 2006 akianza secondary School , Spoks alionekana kuanza kupenda sana muziki, hivyo alianza kuimba na kurudia baadhi ya nyimbo za wasanii waliokuwa wanavuma ndani na nje ya nchi kwa kipindi hicho na kuwa anaimba katika sehemu tofautitofauti.

Mwanzo wa Spoks ulikuwa mgumu sana sababu ya kukosa pesa ya kuingia studio ku Record, mwaka 2009 ndipo Spoks amefanikiwa kuingia Studio akaricodi wimbo wake wa kwanza uitwawo » WARAMBANIYE » katika Studio ya Maibobo Record na baada ya uwo wimbo Spoks ameweza ku record nyimbo zingine ila kwa bahati mbaya nyimbo hizo hazikuweza ku hit .

Mwaka 2011,baada ya hapo Spoks alisimamisha kidogo music akaingia kwenye mambo ya u DJ , alikuwa na Studio yake MUTANGA Nord ndipo alikuwa akifanyia kazi akitambulika kwa Jina la DJ Spoks.
Mwaka 2013, ndipo Spoks amerudi kwenye game la muziki, akafanya wimbo NDATEMUTSE akimshilikisha 19th na hapo Spoks ndipo akaweza kujulikana sehemu mbali mbali, baada ya hapo akafanya nyimbo zingine kama SIKO NABISANZE, AGAKUKU, NZOBIKI MURI KAZOZA, BURUNDI na zinginezo…

Mwaka 2014 Katika tamasha TOPTEN TUBE MUSIC AWARD ambayo ilikuwa ikiandaliwa na RADIO BONESHA FM, SPOKS aliweza kupewa TUNZO (AWARD) kama NEW UPCOMING ARTIST.
Huyo huyo mwaka wa 2014 , wimbo wake wa SIKO NABISANZE umeweza kupata na fasi ya tatu katika ISANGANIRO AWARD TUNZO ambayo inaandaliwa na kituo cha RADIO ISANGANIRO kila mwaka.

Mwaka 2015 Spoks amepata nafasi ya kushiriki kwa mara nyingine kwenye TUNZO ZA ISANGANIRO AWARD 5th Edition , na kuibuka Mshindi kwa sababu ya wimbo wake uliopewa jina la BURUNDI.

Spoks hivi karibuni anatarajia kuachia Album yake ya kwanza inayobeba jina la NDAKUMBUYE IWACU ( Missing home ).
Hayo ndio maisha halisi ya SPOKS MAN.
Huu ndio wimbo ambao unatambulisha ALBUM YAKE.

Ikiwa na wewe ni msanii na unataka tuzungumzie maisha yako na kazi zako za Muziki.Usikose kuwasilia nayo kwenda nambari (+257) 75497258 (WhatsApp pia)

Favicon Swahilimedia Maisha halisi ya SPOKS Man Bio