Search in the website:

HABARI ZA ULIMWENGU

China, Japan na Korea Kusini za saini mkataba

27 décembre 2019

China, Japan na Korea Kusini za saini mkataba. Bw. Geng amesema nchi hizo tatu zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika ulinzi wa mazingira, mabadiliko ya hali ya hewa, afya, uzeeni, uvumbuzi, michezo na vijana ili kupanua maslahi ya pamoja. Pia zitashikilia kufungua mlango kwa nje na kulinda kwa pamoja utaratibu wa pande nyingi na biashara huria na […]

Read More

Watu elfu 99 wakamatwa na china kwa hutma za uhalifu wa kutumia simu kwa njia mbaya

26 décembre 2019

Wizara ya Usalama wa Umma ya China imesema, Polisi nchini humo imefungua kesi 118,000 za uhalifu wa utapeli kwa kutumia simu za mkononi na kuwakamata watu elfu 99 wakati wa operesheni ya «Cloud Sword» iliyoanza mwezi Juni mwaka huu. Mkurugenzi wa Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu iliyo chini ya Wizara hiyo Liu Zhongyi amesema, katika […]

Read More

APPLE,MICROSOFT,TESLA,GOOGLE NA DELL za shutumiwa kutumikisha watoto katika migodi ya cobalt.

18 décembre 2019

Shirika la haki za binadamu linashutumu kampuni ya Apple, Microsoft, Tesla, Google na Dell kwa kuchukua fursa ya utumikishwaji wa watoto katika migodi ya cobalt katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kesi hiyo iliwasilishwa Jumapili na Mawakili wa Haki za Kimataifa (IRA) katika korti ya Washington; kwa niaba ya wahasiriwa 14 ambao hawajatambuliwa, ikiwa ni […]

Read More

Kiongozi mmoja wa waasi wa FDLR auwawa mashariki mwa congo ya kidemocrasia

15 décembre 2019

Kiongozi mmoja wa waasi wa FDLR auwawa mashariki mwa congo ya kidemocrasia. Jeshi la jemuhuri ya kidemocrasi ya congo lime muuwa kwa risasi Shukuru Mahigane Paulin kiongozi wa waasi wa ki hutu.Ame uwawa katika operesheni ya sokola2 mashariki mwa congo. toka tarehe disemba 11 Picha ya kiongozi huyo imeanza kuonekana kwenye mitandao ya kijaamii akiwa […]

Read More

Sierra Leone yakumbwa na maafa kisa mvua kubwa

15 août 2017

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na maporomoko ya udongo na mafuriko katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown, imeongezeka na kufikia zaidi ya watu mia tatu. Inaofiwa kwamba miili zaidi iko chini ya vifusi. Jitihada za kuokoa zilisitishwa kwa muda baada ya giza kuingia. Rais Ernest Bai Koroma amesema kupitia televisheni kwamba vituo vya […]

Read More

Mtoto mkubwa wa Trump,Donald Trump junior alifanya mkutano na wakili wa Urusi

9 juillet 2017

Donald Trump junior, mwana mkubwa wa kiume wa Rais wa Marekani, Donald Trump, amekiri kuwa alifanya mkutano na wakili mmoja kutoka Urusi, aliye na uhusiano wa karibu na Ikulu ya Kremlin mwezi Juni mwaka jana. Mkutano huo ulifanyika muda mfupi baada ya babake kushinda uteuzi wa kuwani kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha […]

Read More

Mlango wa Raia wa mataifa ya Waislamu kuingia Marekani wafunguliwa tena

4 février 2017

Jaji mmoja wa Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini Marekani. Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea […]

Read More

Trump awapiga marufuku Wakimbizi wa Syria Marekani

29 janvier 2017

Rais mpya wa Marekani Donald Trump amepiga marufuku wakimbizi wote wa Syria kuingia Marekani hadi wakati anasema serikali yake itakuwa imeweka mkakati mkali zaidi wa kuwakagua wakimbizi wanaotafuta hifadhi nchini humo. Kwa mujibu wa amri hiyo ya Trump, wakimbizi wote wanaofika mipakani mwa Marekani kwa sababu ya kutoroka vita makwao au sababu yoyote nyengine pia […]

Read More

Trump aiomba Israel kusitisha ujenzi katika ardhi ya Palestina

22 décembre 2016

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amelitaka azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kusitisha ujenzi wa makaazi ya Israel katika ardhi ya Palestina. Katika taarifa iliotolewa kabla ya kura hiyo inayotarajiwa baadaye siku ya Alhamisi, Bw Trump amesema kuwa amani haitaafikiwa kupitia hatua ya Umoja wa Mataifa kuweka masharti. Azimio hilo litaagiza […]

Read More

Wabunge wapigana nchini Kenya

22 décembre 2016

Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira katika mji mkuu wa Nairobi, wakisema kuwa baadhi yao walinyanyaswa bungeni mapema asubuhi. Kikao hicho maalum ambacho vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia kilitarajiwa kupigia kura marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo inaruhusu kuhesabiwa kwa kura moja baada ya nyengine katika uchaguzi wa urais mwaka ujao. Serikali […]

Read More

Load more

Share
Share