Lavista 4 octobre 2016
Amnesty International limeyashutumu mataifa tajiri duniani kwa kupuuza jukumu lao kwa wakimbizi likisema yanawahifadhi wakimbizi kidogo na kuwajibika kidogo. Nchi kumi zinzojumuisha 2.5% pekee ya pato jumla la dunia zinawahifadhi zaidi ya nusu ya wakimbizi milioni 21 duniani, inasema ripoti ya shirika hilo. Salil Shetty, katibu mkuu wa Amnesty, ameyataka mataifa tajiri kuwahifadhi wakimbizi zaidi. […]
Lavista 28 septembre 2016
Album ya Adele, 25 imeuza nakala milioni 10 nchini Marekani na kumfanya kuwa mwanamuziki wa Uingereza aliyeuza zaidi katika karne hii. Kufuatia album hiyo iliyotoka November mwaka jana kupata hadhi ya ‘diamond platinum’ yaani kuuza nakala milioni 10, msanii huyo alipewa ngao katika ukumbi wa Madison Square Garden jijini New York, ambako ametumbuiza show sita […]
Lavista 28 septembre 2016
Mchezaji wa klabu ya Manchester City, Yaya Toure amefunguka kuwa wachezaji na mashabiki wanaweza kuumia kufuatia hatua ya shirikisho la soka duniani (FIFA) kuvunja kikosi kazi kilichoundwa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi katika soka. Toure mwenye miaka 33, alikuwa mmoja wa wajumbe katika kikosi kazi hicho kilichoundwa mwaka 2013 kusaidia […]
Lavista 27 septembre 2016
Kundi la wapiganaji wa al-shabab limetoa kanda ya video inayoonyesha kile inachosema ni mwanajeshi wa Uganda aliyekamatwa mwaka mmoja uliopita nchini Somalia. Katika video hiyo ya dakika sita ,mtu mmoja aliyevaa magwanda ya jeshi la Uganda anamtaka rais wa Uganda kumsaidia kuachiliwa huru. Anasema alikamatwa katika uvamizi wa kundi la al-Shabab katika kambi ya majeshi […]
Lavista 27 septembre 2016
Dawa ya kwanza duniani ya kutibu ugonjwa wa kifua kikuu miongoni mwa watoto inatarajiwa kuzinduliwa leo siku ya Jumanne mjini Nairobi. Hadi kufikia sasa,watoto hutumia dawa zinazotumiwa na watu wazima ambazo hugawanywa kusagwa na kutiwa katika maji. Daktari Cherise Scott,mkurugenzi wa maswala ya magonjwa ya watoto katika muungano wa utengezaji wa dawa za TB ,anasema […]
Lavista 27 septembre 2016
Wagombea urais nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wamepambana vikali katika mdahalo wa kwanza wa televisheni ambapo wamepingana katika masuala mbali mbali ikiwemo masuala ya sera, kodi, ajira na uchumi. Kadhalika wamejibizana kuhusu Vita vya Iraq na juhudi za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State. Msimamizi wa mdahalo huo Lester Holt amemwuliza mgombea wa […]
Lavista 27 septembre 2016
Somalia imeanza zoezi la kuwateua wabunge 275, zoezi ambalo linatarajiwa kumalizika tarehe 10 mwezi Oktoba. Wagombea mbalimbali wamekuwa wakionekana mjini Mogadishu, Baidoa na Kismayu wakishiriki kwenye kampeni kuomba uungwaji mkono ili kupata nafasi ya kuingia bungeni. Uteuzi wa wabunge hao wapya unafanywa na wajumbe 51 ambao ni viongozi wa dini, watu wenye ushawishi katika jamii […]
Lavista 26 septembre 2016
Kiongozi wa waasi na aliyekuwa Makamu wa rais nchini Sudan Kusini Riek Machar ametangaza vita vipya dhidi ya serikali ya Juba akiwa nje ya nchi. Machar ambaye yupo jijini Khartoum katika nchi jirani ya Sudan, amesema lengo lake la kutangaza vita ni kutaka kurejea kwa amani, uhuru, demokrasia na utii wa sheria katika nchi yake. […]
Lavista 26 septembre 2016
Milolongo mirefu imeshuhudiwa kwenye benki na vituo vya kutoa pesa, kwenye mji mkuu wa Gabon Libreville wakati wanajaribu kutoa pesa, wakihofia kuwa mzozo wa kisiasa uliopo unaweza kuzua machafuko na ghasia nchini humo. Watu wengine walielezea ghadhabu yao kuwa hawangeweza kutoa pesa zao kwenye benki kisingekuwa kisa hicho na hofu tele waliyonayo. « Benki tena hazitaki kutoa […]
Lavista 26 septembre 2016
Wanajeshi wanne wa Chad wameuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kundi la wanamgambo wa Boko Haram kushambulia kambi yao eneo la kaskazini la mpaka na Niger mwishoni mwa wiki. Nao wanamgambo saba waliuawa wakati jeshi lilijibu shambulizi hilo. Mwaka uliopita Chad ilijiunga kwenye vita dhidi ya Boko Haram amboa walianzisha harakati zao Kaskazini Masharikia […]