Milolongo mirefu imeshuhudiwa kwenye benki na vituo vya kutoa pesa, kwenye mji mkuu wa Gabon Libreville wakati wanajaribu kutoa pesa, wakihofia kuwa mzozo wa kisiasa uliopo unaweza kuzua machafuko na ghasia nchini humo.

Watu wengine walielezea ghadhabu yao kuwa hawangeweza kutoa pesa zao kwenye benki kisingekuwa kisa hicho na hofu tele waliyonayo.

« Benki tena hazitaki kutoa pesa, kwa sababu zinaelewa hali sio nzuri na uchumi uko hatarini, » alisema mwalimu mmoja.

Baadhi ya maduka mjini Libreville yanaishiwa na bidhaa huku familia nyingi nazo zikiishiwa bidhaa muhimu.

Favicon Wawekezaji Nchini GABON watoa pesa zao benki kwa kuhofia machafuko