Wanajeshi wanne wa Chad wameuawa na wengine sita kujeruhiwa baada ya kundi la wanamgambo wa Boko Haram kushambulia kambi yao eneo la kaskazini la mpaka na Niger mwishoni mwa wiki.

Nao wanamgambo saba waliuawa wakati jeshi lilijibu shambulizi hilo.

Mwaka uliopita Chad ilijiunga kwenye vita dhidi ya Boko Haram amboa walianzisha harakati zao Kaskazini Masharikia mwa Nigeria mwaka 2009.

Washambuliaji wa kike wa kujitolea mhanga waliwaua takriban watu 23 na kuwajeruhi zaidi ya 100 katia kituo cha polisi na soko kwenye mji mkuu wa Chad Ndjamena mwezi Julai mwaka 2015.

Favicon Boko Haram waua wanajeshi wanne wa Chad