Muungano wa redio za uvira na Fizi na kamanyola SYMUF, mashariki mwa Drc kivu kusini, waendesha mjadala uliyo kutanisha wana habari wa uvira na fizi,wakuu viongozi wa ki jeshi,polisi,mashirika za ki raia pamaja na raia wa mji wa uvira.Mjadala waendeshwa katika hali ya kusherehekea siku kuu ulimwenguni ya redio inayo yerehekewa kila tarehe 13 february. Kiongozi wa muungano huo bwana Aubert Mwibaceca, ameimbia swahili grands lacs medias ya kuwa  »Kuna umuhimu wa kukaribiana na wasikilizaji wetu wa kila siku ili tuzungumuze ana kwa ana kuhusu namna Vifaa hivi vya mawasiliano vinavyo saidia jamii wa kabila,Dini na mila tofauti kuishi pamoja kwa amani ». Zaidi ya redio ishirini za miji na tarafa za Uvira,Baraka,Fizi,walungu na mwenga, zime tanganza toka hiyo february 12 ujumbe unao alika watu kuishi kwa ummoja. Sherehe hizi zime endeshwa na symuf kwa ushirikiano na la Benevolencija.

Favicon Uvira Drc Muungano wa vyombo vya habari Uvira Fizi na kamanyola wa sherehekea siku kuu ya redio