China imeanzisha Jumapili hii darubini kubwa duniani katika mkoa wa Guizhou, kusini magharibi mwa nchi hiyo. Kikiwa na mduara wa mita 500, chombo hiki cha uangalizi kitaweza kunasa ihara mbalimbali katika pembe zilizo mbali sana ulimwenguni.

Beijing ina matumaini kuwa ina uwezo wa kupata dalili za maisha yaliyo mbali na satari ya dunia.

Darubini hii kubwa duniani imeanza kufanya kazi Jumapili hii kusini magharibi mwa China, kama sehemu ya mradi mkubwa ambapo lengo lake, kwa mujib wa serikali ya Beijing litakua kuchunguza maisha yaliyojaa akili mbali na sayari ya dunia.

Darubini hiyo iliyoitwa na wanasayansi kuwa ni « Five-hundred-metre Aperture Radio Telescope » (FAST), darubini hii imeanza kufanya kazi Jumapili hii mchana, shirika la habari la Xinhua limearifu. Ufunguzi wake rasmi utafanyika Ijumaa 30 Septemba.

Chombo hiki kikubwa, ambacho kinawakilisha sayari yenye mduara wa mita 500, ukiwa sawana viwanja 30 vya soka, kimewekwa katika eneo la kijijini la jimbo la Guizhou,kati ya vijiji vitatau vya Karst. Pamoja na kioo chake kikubwa kinachoundwa na vifaa 4450,kitakacho kuwa na uwezo wa kuchukua ishara kutoka pembe za mwisho wa ulimwengu.

Chombo hiki ambacho kimeanzishwa na kuanza kujengwa mwezi Machi 2011, kiligharimu 165,000,000.

Favicon Darubini kubwa duniani yaanzishwa na CHINA