Shirika la kibinaadamu la Human Rights Watch linasema kuwa vikosi vya usalama ini DR Congo vimewaua takriban watu 34 wakati wa maandamano wiki hii.

Mazungumzo yanayoendeshwa na kanisa katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili kujaribu kumaliza mgogoro katika ya upinzani na rais Joseph Kabila ambaye alikataa kuondoka madarakani wakati muda wake ulipokamilika siku ya Jumatatu.

Kuna ripoti tofauti kwamba watu wengine 17 wameuawa kaskazini magharibi mwa Congo.

Maafisa wa polisi wanadaiwa kukabiliana na wanachama wa kundi moja la madhehebu linaloamini kwamba mwisho wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa mwisho wa dunia.

Wakati huohuo Mamlaka nchini DRCongo imewakamata watu kadhaa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Lubumbashi.

Meya wa mji huo anasema kwamba wanajeshi walikuwa wakiwakamata wahalifu, japo wenyeji wa mji huo wanasema waliokamatwa ni vijana wanaoshukiwa kupinga utawala wa rais Joseph Kabila.

Favicon Watu 34 wadaiwa kufariki katika maandamano DR Congo