Zaidi ya ma mia ya wapiganaji wa CNRD pamoja na FDLR waasi wa Rwanda, wamekamatwa na jeshi
la congo ya kidemocrasia FARDC disemba tarehe tatu 2019 na kupelekwa kwenye kambi ya jeshi la
Fardc pa Kalonge mashariki mwa drc kivu kusini.
Dieudonné Kasereka,msemaji wa jeshi mashariki mwa drc kivu kusini asema ya kuwa ,wamekamatwa
wakiwa na familia zao,wakikadiria kuwa ma mia ya watu waki kimbia mapigano.Mapigano ya
kiendelea eneo la kalehe mashariki mwa congo ,Msemaji wa jeshi la fardc asema ya kuwa ,wapiganaji
wengi wameanza kuweka silaha chini na kujiripoti huku wengine wakiendelea kujificha huku na kule.
Jeshi la fardc wamewaomba raia wa maeneo hayo,kuto kuwapokea waasi na kuwapa makaazi ,bali
washirikiane na vyombo vya usalama ili waweke kando vikundi hivyo vinavyo dhuru usalama kivu
kusini.
Dieudonne Kasereka asema ya kuwa ni mdaa wa kutokomeza vikundi vya kijeshi vya kigeni na vile vya
hapa inchini ili amani na usalama ishuhudiwe.
Jeshi la congo limeanzisha operesheni ya kivita dhidi ya makundi ya kihutu ya CNRD na FDLR katika
mtaa wa Bitale tarafani KALEHE.Imeonekana yakuwa makundi ya wapiganaji hao wameanza kuhamia
maeneo mengine wakiwa na familia zao,yasema shirika la kirai la mahali.
Mapigano hayo,tayari kupekea zaidi ya watu elfu tatu kuyahama makaazi yao yasema 7SUR7.CD.

Chumba cha habari /
swahili media.com

Favicon Wapiganaji wa CNRD pamoja na FDLR wakamatwa na jeshi la FARDC