Serikali ya Ufaransa imechangia kiasi cha Euro 250,000 kwa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP ili wakimbizi nchini Tanzania waweze kupata msaada zaidi wa kifedha.
Msaada huu unadhihirisha mchango wa serikali ya Ufaransa katika kuhakikisha kuna hali ya usalama wa chakula.
Mwezi Desemba mwaka jana, WFP ilianza kusambaza shilingi za kitanzania 20,000 sawa na dola 9 za marekani kila mwezi kwa wakimbizi 10,000 ukiwa ni mpango wa majaribio uliotekelezwa kwa kushirikiana na washirika ikiwemo serikali ya Tanzania na shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
Mchango wa Ufaransa unaiwezesha WFP kuendeleza mradhi huu wa kutoa fedha kwa wakimbizi 10,000 kwa kipindi cha miezi miwili zaidi.

Soma zaidi:http://www.bbc.com/swahili/habari-40484286

Favicon Ufaransa yachangia Euro 250 000 kusaidia wakimbizi Tanzania