Bingwa wa uzani mzito duniani Tyson Fury huenda asipigane tena ,kulingana na afisa wa mauzo katika ndondi ya kulipwa nchini Uingereza.

Fury mwenye umri wa miaka 28 amejiondoa katika pigano la marudiano kati yake na Wladimir Klitschko lililotarajiwa kufanyika Oktoba 29 kutokana na matatizo ya kiafya .

Muingereza huyo ambaye hajapigana tangu kumshinda Klitschko mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita aliahirisha mechi hiyo mnamo mwezi Juni.

« Fury atapokonywa mataji yake na baada ya makabiiano ya kisheria mahakamani, atasema »sitaki tena » ,alisema Hearn.

»Itakuwa makabiliano makubwa na itachukua mwaka mmoja kutatua.Najua kuna maswala nyeti kuhusu afya yake lakini hii ni biashara ».

»Bodi zinazosimamia mataji hayo zimetoshekwa.Ukanda wa uzani mzito duniani ni biashara yao kubwa na hawajapata fedha zozote kutokana na ukanda huo mwaka mmoja sasa ».

Favicon Tyson huenda akasimamisha kupigane tena