Tofy Gas adai kuvunja ukimya wake

Bada ya muda mrefu kidogo akiwa kwenye ukimya ambao ulizua maneno na viulizo vingi kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetambulika kama TOFY GAS,sasa ameamua kuvunja ukimya na kufunguka zaidi .

Akiongea na wandishi wa habari amesema kuwa anatarajia kuachia wimbo wake mwingine baada ya STAY STRONG,NA KWANINI MIMI aliomshirikisha mwanamuziki kongwe wa BONGO FLEVA TID MNYAMA.

amesema kwamba wimbo huo anategemea utampa picha na sifa zingine na jina jpya tena kwa sababu ni wimbo ambao umetengenezwa kwenye mitindo tofauti na ile ambayo tumezoea kwake.

Ameendelea na kusema kuwa zaidi kwenye wimbo huo ameamua kumshirikisha RAPPER FAB LOVE anayetamba kwa kibao chake cha MAGONDE.

Wimbo huo unatarajiwa kuachiwa mnamo TAREHE 2/NOVEMBA/2017.

STAY TUNED.

Endelea kusubiria kibao hicho zaidi ukiburudika na wimbo wake wa KWANINI MIMI.Usisahau kushare na wenzako kama kawaida yetu.

Favicon Tofy Gas adai kuvunja ukimya wake