Swahilimedia Wimbo wa Wangu by Natacha feat Shebbah watarajiwa kuimbwa Coke Studio Africa
Baada ya kuwa wimbo wa WANGU wa kwake NATACHA akimshirikisha SHEBBAH wa UGANDA kuachiwa nje na kupokelewa kwa shangwe kubwa na sapoti nyingi sana.
Sasa wimbo huo unatarajiwa kuimba COKE STUDIO AFRICA na SHEBBAH.

Kwa mjibu wa Mwanahabari wa NATACHA ,DJ RAPHAN amesema kwamba tayari washaweka makubaliano na SHEBBAH kuwa wimbo huo utaibwa kwenye show inayofanyika COKE STUDIO AFRICA.

Tumepata nafasi nzuri sana ya kumuuliza DJ RAPHAN ni kitu ganai ambacho wanategemea kama faida kwa wimbo huo endapo utaimbwa COKE STUDIO AFRICA?
Ametufungukia sana na kusema kuwa lengo lao zaidi ni kupanua muziki wa Burundi ufike kimataifa zaidi na kumtambulisha NATACHA pia.
Ameongeza akisema kuwa mbali na kuwa NATACHA hatashiriki kwenye kuimba wimbo huo COKE STUDIO lakini wanategemea makubwa kutoka kwa SHEBBAH kwa maana WIMBO HUO na yeye ameuchukulia kama wimbo wake pia na kuweka ahadi ya kuiweka wimbo huo kwenye ALBUM yake ambayo iko inaanfaliwa kuachiwa siku za mbele.

endelea kuburudika na wimbo huo wa WANGU BY NATACHA FEAT. SHEBBAH.Zaidi kuwatumia na wengine habari hii.

Favicon Swahilimedia Wimbo wa Wangu by Natacha feat Shebbah watarajiwa kuimbwa Coke Studio Africa