Swahilimedia Jina la Irungu wimbo wake Titus Da Sailor laleta utata kwa mashabiki
Baada ya kuachia wimbo wake wa IRUNGU wimbo wake MWANAMUZIKI CHIPUKIZI TITUS DA SAILOR,sasa utata na gumzo nyingi vimeanza kwa mashabiki na wapenzi wa kibao hicho.

Ishu nzima ilianza wakati mwanamuziki huyo akiutambulisha wimbo wake,ambapo watu wengi hasa watangazaji ambao walikuwa wamealikwa kwenye utambulishio huo walionekana kutoa maoni yao zaidi wakipendelea kuwa wimbo huo ungepewa jina la INYAMBUKIRA ambalo ndio jina ambalo linarudiliwa sana kwenye wimbo huo.

Baadae mwanamuziki huyo alijitetea vilivyo na kudhibitisha ni kwanini yeye alipendelea wimbo huo ubakie kuitwa IRUNGU.

Mashaka na utata sasa vimekuja kwa mashabiki na kila mtu anayetazama na kusikiliza wimbo huo wengi zaidi wakipendelea kuwa wimbo huo ungepewa jina la INYAMBUKIR kitu ambacho mmiliki wa wimbo huo anakipinga sana.

Tazama na sikiliza wimbo huo hapa chini kisha na wewe aqchia maoni yako ili tujue msimamo wako pia.
Usisahau kushare na wengine habari hii.

Favicon Swahilimedia Jina la Irungu wimbo wake Titus Da Sailor laleta utata kwa mashabiki