Serikali na upinzani DRC washindwa kutilia sahihi mgawanyo wa madaraka
Raisi wa maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC Askofu Marcel Utembi, akiwa na katibu mkuu wa CENCO, Donatien Nsholé,
AFP/JUNIOR D.KANNAH

Serikali na makundi ya upinzani nchini DR Congo wameshindwa kutiliana saini makubaliano ya kugawana mamlaka,hatua iliyopaswa kufanyika tarehe 28 Januari.

Maaskofu wa kanisa katoliki Cenco wanaoratibu mchakato huo wa kisiasa chini DRC wamesema bado pande hizo zinatofautiana katika hoja tatu likiwemo suala la uteuzi wa waziri mkuu,ambapo upande wa serikali unataka majina ya wagombea watano yawasilishwe ambao miongoni mwao raisi wa jamuhuri atamteua kuwa mkuu wa serikali jambo ambalo halikufanikiwa kupitishwa.

Pande hizo mbili zimetumia karibu mwezi mzima kuafikiana hatma hiyo.

Makubaliano hayo yalioafikiwa chini ya usimamizi wa maaskofu wa kanisa katoliki yanaweka utaratibu wa kuondoka kwa rais Joseph Kabila ambaye muda wake wa utawala ulikamilika mwaka jana.

Favicon Serikali na upinzani DRC washindwa kutilia sahihi mgawanyo wa madaraka