Aliyekuwa nahodha wa kikosi cha soka nchini Cameroon Rogobert Song hatimaye amepata fahamu ,kulingana na mamlaka.

Beki huyo wa zamani wa timu ya Liverpool na West Ham sasa ameanza kupumua bila ya usaidizi ,siku mbili baada ya kukimbizwa hospitalini akiwa katika hali mahututi.

Song mwenye umri wa miaka 40 alilazwa katika hospitali ya Younde siku ya Jumapili baada ya kupoteza fahamu.

Mchezaji huyo ambaye ni shujaa wa kitaifa nchini Cameroon ,alilishindia taifa lake vikombe viwili vya bara Afrika na kushiriki katika michuano minne ya fainali za kombe la dunia

Alitarajiwa kusafirishwa hadi mjini Paris kwa matibabu zaidi chini ya agizo la rais wa Cameroon Paul Biya.

« Baada ya rais kuelezewa ,alitoa agizo kwa wizara ya afya kufanya kila iwezalo ili kumsafirishwa ng’ambo » ,alisema msemaji wa serikali Issa Thsiroma.

»Tunashukuru vifaa vya hali ya juu vya matibabu na utaalam tulionao nchini Cameroon,tumefanikiwa kudhibiti hali yake,ili aweze kusafirishwa »,aliongezea msemaji huyo.

Favicon Rigobert Song apata fahamu