Gazeti la Daily Nation la nchini Kenya linasema kuwa raia wawili wa Iran wamekamatwa kwenye mji mkuu Nairobi.

Watu hao ni kundi la pili la raia wa Iran kukamywa nchini Kenya kwa ushukiwa kunpanga njama ya kutaka kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Mwezi Juni mwaka 2012 utawala nchini Kenya uliwakamata Ahmad Mohammed na Sayed Mousavi wa kutengeneza vilipuzi ambavyo ilidaiwa walinuia kuvitumia kwa mashambulizi.

Walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2013 lakinio vifungo vyao vilibatilishwa na kuwa vya miaka 15 baada ya wao kukata rufaa.

Mwezi Novemba mwaka uliopita wakenya wawili Abubakar Sadiq Louw wa umri wa miaka 69, and Yassin Sambai Juma 25, waliakamatwa baada ya kushukiwa kulifanyia ujasusi shirika la ujasusi la Iran.

Favicon Raia wawili wa Iran wakamatwa wakipiga picha Kenya Nairobi