Mtoto mkubwa wa Trump Donald Trump junior alifanya mkutano na wakili wa Urusi
Donald Trump junior, mwana mkubwa wa kiume wa Rais wa Marekani, Donald Trump, amekiri kuwa alifanya mkutano na wakili mmoja kutoka Urusi, aliye na uhusiano wa karibu na Ikulu ya Kremlin mwezi Juni mwaka jana.
Mkutano huo ulifanyika muda mfupi baada ya babake kushinda uteuzi wa kuwani kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican.
Kijana mkwe wa Trump Jared Kushner, na aliyekuwa mwenyekiti wa kikosi cha kumfanyia Trump Kampeini za kisiasa, Paul Manafort, pia walihudhuria mkutano huo.
Donald Trump Junior anasema kuwa mkutano wake pamoja na wakili huyo wa Urusi Natalia Vesel-nits-kaya, ulikuwa mfupi mno, na ulilenga swala la kuwapa hifadhi watoto mayatima.
Mwendesha mashtaka maalum kwa sasa anaendelea na uchunguzi kubaini iwapo Urusi ilimsaidia Trump kushinda uchaguzi huo.

Favicon Mtoto mkubwa wa Trump Donald Trump junior alifanya mkutano na wakili wa Urusi