Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania waliouawa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Miili hiyo imesafirishwa kwa ndege za Umoja wa Mataifa kutoka nchini DR Congo.
Waliuawa wakati wa shambulio lililotekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Soma zaidi.

Favicon Miili ya wanajeshi waliouawa DRC yarejeshwa Tanzania