Mchekeshaji wa Afrika Kusini anayefanyika kazi nchini Marekani, Trevor Noah, ametangazwa kuwa mshereheshaji wa tuzo za mwaka huu za MTV MAMA.

Awali Idris Sultan, Basket Mouth (Nigeria), Idris Elba (Uingereza) na Kevin Hart (Marekani) walikuwa miongoni mwa washereheshaji wengine waliokuwa wanafikiriwa.

Tuzo hizo zitafanyika October 22, 2016, kwenye ukumbi wa Ticket Pro Dome, Johannesburg, Afrika Kusini. Yemi Alade, Ycee, Cassper Nyovest na Alikiba wanatarajiwa kuwasha moto kwa kutumbuiza.

Mchekeshaji Trevor Noah atangazwa kusherehesha kwenye tuzo za MTV MAMA

Rapper wa Afrika Kusini, Nasty C na muimbaji wa nchi hiyo, Babes Wodumo na mwanamuziki kutoka nchini Tanzania ALIKIBA nao watatumbuiza. Majina ya wasanii watakaowania tuzo hizo mwaka huu yatatajwa, jijini Johannesburg mwezi huu.

Favicon Mchekeshaji Trevor Noah atangazwa kusherehesha kwenye tuzo za MTV MAMA