Ujumbe wa mahakama, wawekwa kwa ombi la jamii ya Banyamulenge waishio nchini DRC na inje ya nchi, ni kwenda Minembwe kukusanya malalamiko kutoka kwa wahasiriwa wa wimbi la vurugu ambalo lime shuhudiwa miezi kadhaa kwenye milima ya nyaja za juu jimboni kivu-kusini.

Katika kibarua kilicho asilishwa kwenye vyombo vya habari na ku sainiwa mnamo Januari 6 huko Brussels, London na New York, mawakili Bernard Maingain na Jean-Paul Shaka, wanaarifu kwamba Banyamulenge (Wa tutsi wa Kivu ya Kusini) wanaoishi Kongo na wale waishio inje,wana pinga kwa njia halali uharibifu unoafanywa kwa jamii ya Banyamulenge iishio Kivu ya Kusini .
wana taja ukeukwaji wa haki zao unapelekea nyumba zao kuchomwa moto, kuharibika kwa shamba zao,na mifugo.
Kwa upande wa wawakili,virugu hizo zinaonesha dhahiri picha ya halisi iliyo wakabili wa tutsi inchini Rwanda mnamo miaka 1950.
Hali hii ya vurugu yaelekea kwenye mauwaji ya kimbari na ambayo ni lazma kutumia njia iliyo bora ili kusimamisha hali hiyo.

Favicon Mawakili waasilisha malalamiko ya Jamii ya Banyamulenge