Amnesty International limeyashutumu mataifa tajiri duniani kwa kupuuza jukumu lao kwa wakimbizi likisema yanawahifadhi wakimbizi kidogo na kuwajibika kidogo.

Nchi kumi zinzojumuisha 2.5% pekee ya pato jumla la dunia zinawahifadhi zaidi ya nusu ya wakimbizi milioni 21 duniani, inasema ripoti ya shirika hilo.

Salil Shetty, katibu mkuu wa Amnesty, ameyataka mataifa tajiri kuwahifadhi wakimbizi zaidi.

Shetty amesema Uingereza « mfano wa kusikitisha » kwa kushindwa kuwajibika.

Uingereza imewapokea wakimbizi 8000 wa Syria tngu 2011 kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Marekani imewapokea 12,000 pekee.

Na kwa mujibu wa data ya hivi karibuni ya shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi, hakuna wakimbizi waliopokewa China, Uusi na katika mataifa ya kiarabu.

Kwa kulinganisha, Jordan, iliyo na pato jumla la 1.2% pekee, kiwango cha Uingereza imewapokea wakimbizi 655,000 wa Syria.

Uturuki imewakubali zaidi ya watu milionimbili na nusu, Pakistan milioni 1.6; na Lebanon zaidi ya milioni 1.5.

« Nchi kidogo zimeachwa kuwajibika pakubwa kutokana na kuwa ni jirani tu na mataifa yanayokumbwa na mzozo, » amesema Bwana Shetty.

Ameongeza: « Iwapo tutagwanya jukumu hili, mfano nchi 60 kati ya 90 zikagawanya jukumu hili, tungekuwa katika hali tofauti. Ni tatizo kubwa lakini linaweza kutatulika. »

Matifa mengine yalio na idadi kubwa ya wakimbizi ni:

  • Iran (979,400)
  • Ethiopia (736,100)
  • Kenya (553,900)
  • Uganda (477,200)
  • Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (383,100)
  • Chad (369,500)

Wakimbizi na wahamiaji wanaendelea kuhatarisha maisha yao wakijaribu kuingia Ulaya.

Jumatatu Italia iliratibu jitihada za uokozi wa watu 2,600 kutoka pwani ya Libya.

Favicon Mataifa tajiri lsquo yanapuuza rsquo jukumu lao kwa wakimbizi 8211 Amnesty