SILAHA Mashariki wa DRC Mai Mai 63 wajisalimisha

Wapiganaji 63 wa kukindi cha Nyatura waliji salimisha kwa jeshi la jemuhuri ya kidemokrasia ya kongo pa masisi mashariki mwa inchi hiyo.Msemaji wa kijeshi sokola ya pili, meja  Ndjike Kaiko Guillaume,amejulisha hivyo  mwanzoni mwa wiki hii January 13.

Msemaji huyo wa kijeshi asema ya kuwa,wapiganaji hao ni mabaki ya kikundi cha Nyatura Kikingi waliokuwa katika mtaa wa Nyamaboko2 ambao walikuwa na shirikiana na kikundi cha mai-mai.

Wakati waku jisalimisha,wali onesha silaha 13 aina ya AKA47 na mmoja ya RPG7 na kuziweka mikononi mwa regimenti ya 3410 pa kikoma katika secta ya Katoyi mtaani Nyamaboko2.

Toka octoba 2019,jeshi la drc wame anzisha operesheni ya vita katika maeneo zinazo dhibitiwa na waasi mashariki mwa inchi ili kurejesha amani na tegemeo ya kuishi katika maeneo hayo.Jeshi la drc laendelea kuomba viongozi wa makundi za kijeshi wafikirie namna wanaweza changia kuleta usalama mashariki  mwa inchi.Makundi mengi ya kijeshi yaonekana kujibu ombi hilo na tayari yameanza kuweka silaha chini na kujiunga na jeshi la jemuhuri ya kidemokrasia ya kongo.

Favicon Mashariki wa DRC Mai Mai 63 wajisalimisha