Kiongozi wa upinzani nchini Kenya,Raila Odinga ametangaza kuwa hayupo tayari kushiriki marudio ya uchaguzi mkuu wa urais nchini humo tarehe 17 mwezi October.

Amesema kuwa anataka kuwepo mikakati ya kisheria na kikatiba inayohitajika,kabla ya yeye kukubali kushiriki uchaguzi huo.
Odinga pia anataka tume ya uchaguzi kufanyiwa mabadiliko kwanza kwa sababu imeshawekewa mashaka na mahakama ya juu kwa kuendesha uchaguzi kwanjia ambayo haikuwa nzuri ambayo ilisababisha kufutiwa mbali matokeo ya awali.

Favicon MARUDIO YA UCHAGUZI KENYA