Muungano mkuu wa upinzani nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Congo unasema kuwa zaidi ya watu 50 waliuawa wakati wa mandamano ya kumpinga rais Joseph Kabila siku ya Jumatatu mjini Kinshasa.

Mmoja wa walioshuhudia anasema polisi waliwafyatulia risasi waandamanaji.

Upinzani umevilaumu vikosi vya usalama kwa kutumia risasi dhidi ya maandamano yanayotaka kutangwazwe tarehe ya uchaguzi wa urais.

Upinzani umeitisha maandamano zaidi leo Jumanne.

Maandamano ya upinzani DRC yasababisha vifo vya watu zaidi ya 50

Serikali ya DRC iliwalaumu waandamanaji waliokuwa wamejihami na kusema waliouawa ni watu 17 wakiwemo polisi watatu.

Waziri wa mambo ya ndani Evariste Boshab amesema mmoja wa maafisa hao wa polisi aliuawa kwa kuchomwa moto akiwa bado yu hai.

Kuna wasiwasi kuwa rais Joseph Kabila ana njama ya kutaka kusalia madarakani baada ya kumalizika kwa muhula wake mwishoni mwa mwaka huu.

Maandamano ya upinzani DRC yasababisha vifo vya watu zaidi ya 50

Nikukumbushe kuwa machafuko hayo  katika mji mkuu yamesababisha hadi shure nyingi kufungwa na biashara kusimama huku raia wakidai kuwa njaa itakuja kuwaua endapo hali hii itaendelea kuongezeka kwa kasi.

Favicon Maandamano ya upinzani DRC yasababisha vifo vya watu zaidi ya 50