Kampuni ya Microsoft imeshtumiwa na kundi la haki za wateja la Consumer Rights dhidi ya programu yake ya Windows 10.

Kundi hilo limesema limepokea mamia ya malalamishi kuhusiana na uboreshaji wa programu hiyo .

Watumiaji wa programu hiyo wanalazimika kulipia komputa zao ili zirekebishwa kutokana na faili kupotea.

Hatahivyo Microsoft ilitetea programu hiyo ya Windows 10 na kusisitiza kuwa imekuwa ikitoa usaidizi kupitia mtandaoni na vilevile kwa simu.

Imeongezea kwamba itawasaidia watu kupata programu yenye manufaa na yenye usalama dhabiti, kulingana na msemaji wa kampuni hiyo.

Lawama za watumiaji wa Progamu ya Windows 10

Kundi hio limesema watumiaji wamekuwa wakilalamikia ujumbe uliokuwa ukijitokeza kwenye tarakilishi na simu zao kila mara, kuwahimiza kuboresha programu hiyo mbali na programu hiyo ya Windows 10 kujiweka yenyewe bila idhini ya mtumiaji.

Pia kumekuwa na malalamiko kuhusiana na huduma mbaya kwa wateja wake,pale wanapohitaji msaada kutoka kwa kampuni hiyo.

Programu hiyo ya windows 10 ilizinduliwa mwezi Julai mwaka 2015, na hutumika katika tarakilishi,simu aina ya smartphone, na vifaa vya kusikilizia sauti vya HoloLens.

Lawama za watumiaji wa Progamu ya Windows 10

Favicon Lawama za watumiaji wa Progamu ya Windows 10