Kundi la wapiganaji wa al-shabab limetoa kanda ya video inayoonyesha kile inachosema ni mwanajeshi wa Uganda aliyekamatwa mwaka mmoja uliopita nchini Somalia.

Katika video hiyo ya dakika sita ,mtu mmoja aliyevaa magwanda ya jeshi la Uganda anamtaka rais wa Uganda kumsaidia kuachiliwa huru.

Anasema alikamatwa katika uvamizi wa kundi la al-Shabab katika kambi ya majeshi ya Afrika katika mji wa Janale,ambapo anasema kwamba kati ya wanajeshi 40 hadi 50 waliuawa.

Kiongozi wa jeshi la Uganda amesema kuwa hajaona kanda hiyo,na wanatumia kila njia kuhakikisha kuwa mwanajeshi huyo ameachiliwa.

Favicon Kundi ya wapiganaji la Al Shabab latoa video ya mwanajeshi wa Uganda