Kipindi cha mvua si raisi kutumia  barabara kutoka tarafani uvira kulekea tarafani fizi.

Mvua zinapo nyesha ,watumiaji wa barabara hiyo ,waendesha gari,piki piki pamoja na wafanya biashara  hupitia matesNvuaMakobola scaled Kipindi cha mvua si raisi kutumia barabara kutoka tarafani uvira kulekea tarafani fizi

Kwa sasa si rahisi kutumia barabara ukitokea Tarafa la Uvira kuelekea tarafa la fizi.Gari zina shuhudiwa kuanguka maeneo ya katungulu huku zingine ziki ziwilika kutokana na ubovu wa barabara.

Mwishoni mwa wiki iliyopita ,mlolongo wa gari uli zuwiliwa kwenye daraja la sanza kutokana na mmomonyoko wa ardhi .Watumiaji wa barabara hiyo wana lalamikia serekali ya jimbo kuto jali barabara inayo faidia serekali na ambayo ni tegemeo kwa wanaichi wengi.

Muandishi wa Swahili medias ametembelea maeneo hayo akishudia namna maji ya mito ya haribu sehemu nyingi za barabara.

Wanaichi wanahofia sana kipindi hiki ambacho watalaam wa hali ya hewa wanasema yakuwa mvua itakuwa nyingi Afrika mashariki<<Hatujuwi tutaishi namna gani siku hizi.Tuna mashaka kwa kuwa wana tueleza mvua itakuwa kali.Hii barabara ni mbaya sana wakati wa mvua,kuna watu wanafariki kwa ajali za barabara na wengine hubaki maskini kipindi hawana njia ya kupitisha biashara vyao>>

Waendesha gari hujuiliza hadi sasa, kwa nini barabara hiyo hia tengenezwi ila wao waendelea kutowa pesa kwa shirira linalo husika na kukarabati barabara,FONER<<Kila gari inayo tokea uvira kuelekea tarafa la fizi, hulipa pesa zaidi ya dolla kumi.Ukihesabu gari zinazo safiri kwa siku na kujumuhisha kwa mwezi utaona kwamba shirika hilo lina ingiza kiwango kikubwa cha pesa.Ni miaka kadhaa shirika hilo lipo ila hatuja wahi kushuhudia umuhimu wao kwetu>>.

Macho ya wanaichi yaiangalia serekali ya jimbo pamoja na serekali kuu ,ili wafikiri lolote kuhusu barabara hiyo inayo waingizia ma millioni ya dolla na ambayo ina changia kwa kiasi kikubwa kwa uchumi wa wanaichi mashariki mwa Congo.

Chumba cha habari/

Swahilimedias.com

Favicon Kipindi cha mvua si raisi kutumia barabara kutoka tarafani uvira kulekea tarafani fizi