KAGAME ET FELIX Inchi ya Rwanda yapongeza serekali ya drc katika operesheni ya vita inayo endesha dhidi ya waasi wahutu FDLRRwanda yaunga mkono jeshi la la jemuhuri ya kidemokrasia ya kongo katika mapigano ya kusaka  waasi wa wahutu wanao onekana inchini drc.waasi hao wanashutumu Kigali na Kinshasa kwamba wana shirikiana katika « kuwauwa », na Rwanda kwa kutaka kuigawa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kikosi cha jeshi la Kongo ya kidemokrasia kina wafuatilia waasi wa Democratic Front for Liberation of Rwanda (FDLR) katika majimbo mawili,kivu kaskazini na kivu kusini. « Asante kwa jeshi la Drc, siku za FDLR zimehesabiwa, » Waziri wa Rwanda anaye simamia Afrika Mashariki Olivier Nduhungirehe alisema kwenye Twitter.  Rwanda ilikuwa tayari ime shangilia mnamo Septemba kifo cha mkuu wa FDLR Sylvestre Mudacumura, kilichotangazwa na jeshi la Drc, moja ya ishara za joto la kidiplomasia kati ya Kinshasa na Kigali.  FDLR inawakusanya washiriki wa zamani wa Kikosi cha Silaha cha Rwanda (FAR) na wanamgambo waliokimbilia Kongo mashariki baada ya mauaji ya Watutsi 800,000 mnamo 1994. Kigali ina washutumu kwa uhalifu. Katika taarifa ya Jumapili, FDLR ililaani « makubaliano yaliyofanyika » kati ya Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi .

Favicon Inchi ya Rwanda yapongeza serekali ya drc katika operesheni ya vita inayo endesha dhidi ya waasi wahutu FDLR