Idadi kubwa ya mai mai yajiunga na FARDC ili kuwapiga ADF tarafani Beni

IMG 20190426 WA0003 Idadi kubwa ya mai mai yajiunga na FARDC ili kuwapiga ADF tarafani Beni

Idadi yao inakadiriwa kuwa 707 wengi wakiwa wa kikundi uhuru.wametoka porini jioni disemba tarehe inne na kujiunga na jeshi la jemuhuri ya kidemocrasia ya congo FARDC.Muhusu Uhuru kiongozi wa wapiganaji hao,asema ya kuwa wamejitolea kuitumikia inchi yao na kuomba wapiganaji wengine wanao salia porini kutoka  ili wapiganishe wapiganaji wa ADF wanao sumbua wanaichi na kusababisha mafaa ya watu zaidi ya elfu tatu mashariki mwa congo katika mji na tarafa la Beni toka 2014.Kiongozi wa mai mai atowa wito kwa wapiganaji wa ADF  kuacha huru ardhi ya congo kabla vita kali haija endeshwa dhidi yao.

Mukulu ,Kanali wa kijeshi FARDC katika eneo la Beni ,anasema kufurahishwa na hatua iliyo chukuliwa na mai mai kwani alifikiri yakuwa mapigano atakayo yaendesha yanahusu kuwa piga mai mai pamoja na ADF ila kwa sasa ni tofauti.Kutokana na kujiunga kwao kwa lengo la kupiganisha ADF,mai mai wanatolewa mafunzo ya kijeshi kabla wawekwe kwenye musafara wa mapigano.

Chumba cha habari/

Swahilimedias.com

Favicon Idadi kubwa ya mai mai yajiunga na FARDC ili kuwapiga ADF tarafani Beni