ICC yaombwa kugeuzia macho yake Beni-Drc.

KIONGOZI WA MAHAKAMA YA ICC ICC yaombwa kugeuzia macho yake Beni Drc

Mashirika ya kiraia nchini DRC yaomba muendesha mashtaka kwenye mahakama ya kimataifa ICC kugeuzia macho yake wiyalani Beni mashariki mwa congo ili kuwa fugulia mashtaka wanao husika kushiriki kwa mbali na kwa karibu katika mauwaji ya raia mashariki mwa congo ya kidemocrasia.

Wakati wa mkutano mkubwa wa nchi wanachama wa Mahakama ya ICC uliofanyika mjini Hague nchini Uholanzi ndipo wito huo watolewa.

Kiongozi wa mashirika za kirai inchini Drc, Joseph Dunia Ruyezi ,asema kuwa anataka ofisi ya kiongozi wa mashtaka kuanzisha mara mmoja uchunguzi kuhusu wanao husika kwa mbali ao kwa karibu katika mauwaji ya wanaichi wa BENI.

Toka 2014 idadi kubwa ya raia wa Beni tayari kupoteza maisha wakishambuliwa na ku uwawa kwa panga ao kwa silaha za moto na watu wanao aminiwa kuwa waasi wa ADF Nalu.

Mashirika za kiraia katika mji wa Uvira jimboni kivu kusini ,wameiambia swahilimedias ya kuwa hali hiyo imefanya raia wa beni kuwa wenye kukosa furaha kila kukicha.Wameomba serekali ya DRC kuchukuwa jukumu lake.

Hali ikiwa yenye kusikitisha,shuguli zikiendelea kunyumbishwa na usalama mdogo ku kumba eneo la BENI, jeshi la serikali ya drc na lile la kulinda amani MONUSCO limetangaza operesheni ya pamoja dhidi ya makundi ya waasi mashariki mwa inchi hiyo.

Hata operesheni hiyo ya vita kutangazwa,mauaji yanaendelea kuripotiwa kila wiki wilayani Beni, huku wakaazi wakiishi kwa hofu na mashaka na wengine washindwa kwenda kazini.

Chumba cha habari /

Swahilimedias.com

Favicon ICC yaombwa kugeuzia macho yake Beni Drc