Search in the website:

  • Home
  • / Events
  • /
  • / Rais Magufuli aagiza mawaziri wa zamani wa wizara ya nishati wachunguzwe

2017-06-12

Rais Magufuli aagiza mawaziri wa zamani wa wizara ya nishati wachunguzwe

Event info

Date: 2017-06-12

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameagiza vyombo vya usalama nchini humo kuwachunguza mawaziri wa zamani wa wizara ya nishati na madini waliotajwa kwenye ripoti ya kamati ya pili ya wanasheria na wachumi, iliyochunguza mchanga wa madini uliozuiliwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Rais Magufuli amesema haya wakati akipokea ripoti ya kamati ya pili iliyohusisha wachumi na wataalamu wa sheria kuchunguza mchanga wa madini ulioko kwenye makontena yaliyozuiliwa kwenye maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania.

Kamati hii pia baada ya kueleza kwa kina hasara iliyotokana na usafirishaji wa mchanga huu toka mwaka 1999 ilipendekeza mambo 20 ambayo ilitaka Serikali iyafanyie kazi ili kuiepusha nchi na hasara zaidi inayotokana na ukwepaji kodi unaofanywa na makampuni hayo pamoja na mikataba ambayo haina maslahi kwa nchi. Soma zaidihttp://sw.rfi.fr/eac/20170612-rais-magufuli-aagiza-mawaziri-wa-zamani-wa-wizara-ya-nishati-wachunguzwe

Favicon Rais Magufuli aagiza mawaziri wa zamani wa wizara ya nishati wachunguzwe
Share
Share