Search in the website:

2023-06-07

Hatutakubali kuchelewesha matokeo ya uchaguzi

Event info

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekataa katakata wito uliotolewa na Muungano wa Afrika AU kucheleweshwa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais.

Muungano wa Ulaya AU unasema kuwa una wasiwasi mkubwa kuhusu uadilifu wa matokeo ya mapema ambayo yalimpatia ushindi Felix Tshisekedi.

Kiongozoi mwengine wa upinzani Martin Fayulu ameitaka mahakama ya kikatiba kufutilia mbali matokeo hayo akidai kwamba ndiye mshindi wa uchaguzi huo.

DR Congo imetakiwa kuchelewesha matokeo ya uchaguzi
Washukiwa 5 wa shambulio la Dusit wawasilishwa mahakamani
Chura mpweke duniani apata mchumba
Ni wazi kwamba wito wa AU wa kufutilia mbali matokeo hayo umeikasirisha serikali.

Msemaji wa serikali Lambert Mende amesema kuwa mahakama ya kikatiba ilikuwa huru na hakuna mtu mwenye haki ya kuielekeza.

Muungano wa Ulaya unasema kuwa mwenyekiti wake , rais wa Rwanda Paul Kagame na viongozi wengine wataelekea Kinshasa kutafuta suluhu ya mgogoro huo.

Bwana Mende alisema kuwa ujumbe huo unakaribishwa lakini akasisitiza kuwa matokeo hayo ya baada ya uchaguzi hayatabadilishwa.

Hiyo inamaanisha kwamba kuapishwa kwa Felix Tshisekedi kutafanyika katika kipindi cha siku chache zijazo iwapo mahakama ya kikatiba itaunga mkono ushindi wake.

Soma zaidi.

 

Favicon Hatutakubali kuchelewesha matokeo ya uchaguzi
Share
Share