DRC-UVIRA/Mto kiliba,hatari kwa wakaazi wa kavimvira

VuaMto DRC UVIRA Mto kiliba hatari kwa wakaazi wa kavimviraZaidi ya familia amsini wamepoteza makaazi yao pa uvira katika kata ya kavimvira mashariki mwa drc kutokana na mvua zinazo endelea kushesha.Mkuu wa kata hiyo ,Justin Mwamba kinyage amesema yakuwa,mto wa kiliba umejaa na kuhama njia yake ya kawaida na  kwenda kufikia kisiwa cha nyangara.Maji yaonekana kongezaka katika kisiwa cha nyangara na kupelekea raia wanao ishi pembezoni kuingiliwa na maji.Nyumba hubomoka huku raia wenye hofu wameanza  mara mmoja kuhama makao yao wakihofia wasije kuangukiwa na ukuta wa nyumba.

Kiongozi wa kata,aomba mashirika za kiutu kujali hali wanayo pitia raia wa maeneo hayo.

Kwani raia wengi wameacha makaazi yao na kupata hifizi kwa majirani.Mashirika za kiraia kwa upande wao ,waendelea kulalamikia serekali ili washurulikie mto huo wa kiliba ambao waweza kuleta majanga katika siku za usoni.

Miezi iliyo pita,raia wengi walipoteza vitu kadhaa na kupelekea watu zaidi ya elfu mmoja kuishi bila maakazi

Kutoka kana na ongezeko la maji katika kisiwa cha Nyangara.

Favicon DRC UVIRA Mto kiliba hatari kwa wakaazi wa kavimvira