Photo kalehe Drc Kivu kusini Zaidi ya watu 2700 wa tarafa la kalehe wahama maakazi yaoDrc-Kivu-kusini/Zaidi ya watu 2700 wa tarafa la kalehe wahama maakazi yao baada ya kuonekana kwa waasi wa Rwanda maeneo hayo.

Waasi wa Rwanda wa CNRD washuhudiwa kuonekana katika tarafa la Kalehe kivu kusini.Hali hiyo,yapelekea zaidi ya raia 2700 kuyahama makazi yao.

Mkuu wa tarafa makamu Bwana  Pascal Cimana, amejulisha vyombo vya habari na kusema ya kuwa wahamijia hao wapitia mateso ya ukosefu wa chakula,wengine huuguwa pasipo kupata msaada wowote wa matibabu mahali wanapo hifadhiwa.

Ameendelea kusema ya kuwa ,amejitaidi ku jadiliana na mashirika za kiutu ili watowe msaada wowote kwa wahamiaji.Ma shirika hizo zime eleza yakuwa wameahidi kujibu ombi hilo  tarehe 15 mwezi huu.

Kwa upande wake,kuna onekana zaidi ya waasi wa Rwanda 300 wa kikundi cha CNRD waonekana waki zinguka zunguka mdaa wa jioni maeneo ya Ngazo na rutali waki shikilia silaha za moto .

Hadi sasa hakuna mapigano yeyote.Kiongozi makamu anafikiri ya kuwa kwamdaa wowote jeshi la FARDC wata endesha shambulizi la vita dhidi ya waasi hao na kuwa tupa inje ya ardhi ya tarafa la Kalehe kivu kusini.

Ifaamike kwamba,mwanzoni mwa mwezi january,kiongozi wa shirika la kiraia pa Kalehe ,Ameweza lalamikia kuhusu uwepo wa waasi wa Rwanda wa kikundi cha CNRD katika tarafa la Kalehe iliyo fanya raia yapata elfu mmoja kuanza kukimbia makaazi yao.

Favicon Drc Kivu kusini Zaidi ya watu 2700 wa tarafa la kalehe wahama maakazi yao