Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo imeuomba ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini, Monusco, kuwaondosha wapiganaji 750 wa Sudan kusini wanaomtii aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan kusini Riek Machar.

Uwepo wa wapiganaji hao katika jimbo la Kivu kaskazini mwa Congo umezusha wasiwasi kwa maafisa wa serikali katika eneno hilo.

Wiki iliopita, maafisa wameiandikia serikali katika mji mkuu Kinshasa wakionya kuwa uwepo wa wapiganaji hao wa Sudan kusini unazusha hatari ya usalam katika eneo hilo.

Serikali sasa imekiomba kikosi cha kulinda amani cha Umoja wamataifa nchini Congo – Monusco kuwaondosha waasi hao kufikia Oktoba 10.

Favicon DRC inataka Monusco kiwaondoe waasi 750 wa Sudan Kusini