Mwanamuziki kutoka Nchini Burundi anayetambulika kama CHRIS BIZ ameumbuka mbele ya mashabiki wake baada ya kuonekana muongo kwa kushindwa kutimiza alichowaahidi.

Kisa na mkasa wa hayo yote ni kuwa jamaa alijitoa nakuwatangazia mashabiki wake kuwa yuko anajiandaa kuachia wimbo mpya ambao utatoka na video,Lakini siku chache baadae jamaa aliumbuka pale alipojikuta wimbo huo ameuachia bila sababu zozote za msingi huku watu wengi wakiulizia video ya wimbo huo na kubaki juu juu.

Kwa maelezo yake CHRIS BIZ alisema kuwa amejikuta hawezi akangoja kufanya video kwa sababu msada aliokuwa akiutengemea umeonekana kuchelewa zaida na kujikuta hawezi kusubiria,ndipo akaona vizuri aachie kwanza wimbo kivyake.

Aliendelea akisema kuwa…

« Sijadanganya mtu yeyote ijapo kuwa nilifanya kinyume na nilivyoahidi,ila nawapa moyo mashabiki wangu video inakuja siku chache tu wataiona »

Hayo ndio maneno aliyoyazungumza mwanamuziki huyo.

Unaweza ukajipakulia wimbo huo na kuusikiliza hapa hapa bila chenga zozote.

Washirikishe wengine.

 

IconSGAudio 509 Chris Biz aumbuka mbele ya mashabiki wake
Favicon Chris Biz aumbuka mbele ya mashabiki wake