P BENI DRC Watu waendelea kuyatoroka makazi yaoZaidi ya watu 100,000 tayari kutoka makazi yao kufuatia machafuko yanayo shuhudiwa wiyalani BENI mashariki mwa Drc.Shirika la UNHCR husika na kuhudumia wakimbizi lasema ya kuwa watu hao walitoroka katika kipindi cha miezi mbili iliyo pita.
Msemaji wa UNHCR, Andrewj Mahecic alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari huko Geneva.

Wanawake,wanaume pamoja na watoto waonekana kutoroka wakielekea katika mji wa Nobili na maeneo Jirani.Watu hao,wanakimbia mashambulizi ya makundi yenye silaha tangu mwezi Desemba mwaka uliopita dhidi ya raia wa miji na vijiji katika eneo la Watalinga, karibu na mpaka na Uganda.

«Raia, pamoja na wale waliotoroka makaazi yao mwezi Novemba na Desemba, ni miongoni mwa wanaolengwa na makundi yenye silaha, ikiwa ni pamoja na waasi wa Uganda wa ADF. Kulingana na viongozi wa eneo hilo, karibu watu 252 wameuawa katika eneo la Beni tangu Desemba 2019. Wengi wamewaambia wafanyakazi wa UNHCR kwamba sasa wanaishi kwa hofu, baada ya kushuhudia mauaji, unyanyasaji wa kijinsia na visa vya utekwaji nyara, » UNHCR imesema.

Favicon BENI DRC Watu waendelea kuyatoroka makazi yao