PICHAYAWATOTO APPLE MICROSOFT TESLA GOOGLE NA DELL za shutumiwa kutumikisha watoto katika migodi ya cobalt

Shirika la haki za binadamu linashutumu kampuni ya Apple, Microsoft, Tesla, Google na Dell kwa kuchukua fursa ya utumikishwaji wa watoto katika migodi ya cobalt katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kesi hiyo iliwasilishwa Jumapili na Mawakili wa Haki za Kimataifa (IRA) katika korti ya Washington; kwa niaba ya wahasiriwa 14 ambao hawajatambuliwa, ikiwa ni familia za watoto waliuoawa katika migodi iliyoanguka kwa mmomonyoko ya ardhi na wengine walio jeruhiwa vikali kwa njia hiyo hiyo. Cobalt ina tumiwa kwa utengenezaji wa betri ya simu za mkononi na magari.

Watoto wenye umri wa chini ya miaka kumi na nane hutumiwa sana ili kusambaza cobalt huku wakilipwa dola  moja ao mbili kwa siku.

Inchi ya DRC ambayo yaonekana kuchukuwa nafasi ya mbele kuwa na rasilimali,raia wa ichini humo wapitia mateso kadha wa kadha na huku inchi ikiendelea kubaki nyuma ki uchumi.

Kampuni zinazo shtakiwa zinafahamu namna cobalt inavyo ipata kutoka drc.Shirika la haki la kibadamu wana ahidi kutaja kampuni zingine husika na kutumia cobalt iyo toka inchini humo.

Mali iyoko mashariki mwa congo,ya pelekea inchi ya drc izame katika mizozo ya vita miaka ishirini sasa.

Chumba cha habari /

swahili media.

Favicon APPLE MICROSOFT TESLA GOOGLE NA DELL za shutumiwa kutumikisha watoto katika migodi ya cobalt