Afisa mmoja mkuu wa chama rasmi cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo amekamatwa alipokuwa akijiandaa kusafiri nje ya taifa hilo,kulingana na AFP.

Bruno Tshibala,naibu katibu mkuu wa chama cha Union for Democracy and Social Progress UDPS alichukuliwa na kuzuia na maafisa wa uhamiaji ambao walimpokonya pasipoti yake ,AFP imeongezea.

Afisa huyo anadaiwa kukamatwa kutokana na jukumu lake la maandamano dhidi ya serikali mwezi uliopita,ambapo takriban watu 17 waliuawa ,kulingana na msemaji wa serikali ambaye aliambia Reuters.

Alikuwa anaelekea nchini Ubelgiji kwa biashara rasmi za kichama kulingana na wenzake,akiongezea kuwa wana wasiwasi kuhusu kuzuiliwa kwake.

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekabiliwa na misururu ya maandamano kuhusu hatua za kutaka kucheleweshwa uchaguzi wa urais.

Tume ya uchaguzi inasema kuwa uchaguzi huenda ukacheleweshwa na kufanyika mwaka 2018,na kuzua hali ya kwamba rais Kabila atasalia madarakani hadi wakati huo.

Kulingana na katiba ya taifa hilo ,hafai kuwania muhula wa tatu.

Favicon Afisa wa upinzani akamatwa akiondoka DRC